Facebook yafungwa Myanmar wakati mkuu wa UN akitoa shinikizo


Majenerali wa kijeshi Myanmar wameziamuru kampuni za intanet kuuzuia mtandao wa Facebook, wakati Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akisema ulimwengu lazima uongeze shinikizo la kuhakikisha kuwa mapinduzi hayo ya kijeshi yanashindwa. 

Mtandao wa Facebook umethibitisha kuwa upatikanaji wa huduma hiyo umeathirika kwa baadhi ya watu na kuziomba mamlaka kuurejesha mtandao huo. 

Taifa hilo la Kusini mashariki mwa Asia limetumbukia tena katika utawala wa moja kwa moja wa kijeshi baada ya kiongozi wa kiraia Aung San Suu Kyi na viongozi wengine wa kiraia kukamatwa Jumatatu na kuhitimisha kipindi kifupi cha kidemokrasia nchini humo. 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres watafanya kila liwezekanalo kuihamasisha jamii ya kimataifa kuiwekea mbinyo Myanmar kuubatilisha mkondo uliochukuliwa na wanajeshi. 

Jeshi la Myanmar limetangaza hali ya hatari kwa mwaka mmoja na kusema litaandaa uchaguzi mpya punde tuhuma zote za udanganyifu katika uchaguzi uliopita zitakapotatuliwa.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi