EU yamtuma mjumbe wake mkuu Moscow kuhusu suala la Navalny


Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell ameelekea leo mjini Moscow akiwa chini ya shinikizo la kuikabili serikali ya Urusi kuhusiana na kufungwa jela kiongozi wa upinzani Alexei Navalny na ukandamizaji dhidi ya waandamanaji. 

Ziara hiyo ambayo ni ya kwanza kufanywa na mjumbe wa ngazi ya juu wa Umoja wa Ulaya nchini Urusi tangu 2017, imezusha shutuma kutoka kwa baadhi ya mataifa ya Ulaya yanayohofia kuwa Urusi itaitumia kama ushahidi kuwa Umoja wa Ulaya unataka kurejesha hali ya kawaida.

 Lakini Borrell amesisitiza kuwa atawasilisha ujumbe wa wazi kwa serikali ya Urusi, licha ya kuipuuzilia mbali miito ya nchi za Magharibi ya kumuwachilia huru mkosoaji mkubwa kabisa wa ndani ya nchi wa Rais Vladmir Putin, Navalny ambaye Jumanne wiki hii alihukumiwa kifungo cha karibu miaka mitatu jela.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi