Taarifa inayoungwa mkono na vyama vyote vya kisiasa nchini Marekani katika Bunge la Congress nchini imeitaka serikali ya Biden kuchelewesha mpango wa kuyaondoa majeshi ya Marekani nchini Afghanistan.
Wanajeshi 25,000 wa Marekani wanatarajiwa kuondoka Afghanistan mwezi Mei, chini ya makubaliano yaliyosainiwa na serikali ya rais wa zamani Donald Trump.
Afisa wa ngazi ya juu wa Marekani, Joseph Dunford, ambaye aliongoza ripoti hiyo, amesema kuwa Taliban inaendelea kuishambulia serikali ya Afghanstan.
Wakosoaji wengi wa mpango huo wanahofia kuwa wapiganaji wa Taliban wanaweza kuchukua mamlaka ya nchi iwapo vikosi vya kigeni vitaondoka.
