
Ni muhimu sana kuwa na ndoto katika maisha yako. Usiishi tu bila kuwa na mipango wala malengo, usiishi tu kama umezaliwa bahati mbaya, lazima uwe na malengo wapi unataka kufika, utapita njia gani na utatumia usafiri gani. Ndoto pekee haiwezi kukufanikisha, lazima kuwe na mikakati madhubuti ya kuisimamia.
Ili uweze kutimiza malengo yako unatakiwa kuzingatia mambo yafuatayo:1. Weka muda maalumu unaotaka ndoto yako itimie. Miezi 6, mwaka, miaka 5, miaka 10, 20? Bila kuweka muda ndoto yako inakuwa haina mashiko.
2. Jiwekee malengo unayopaswa kufikia kwa muda fulani ili kutimiza ndoto yako. Kila mwaka au mwezi uwe na lengo unalotazamia kufikia.
3. Weka mikakati ya kila siku nini unapaswa kufanya ili kufikia ndoto yako na uhakikishe unaifanya.
Endelea kutembelea
Muungwana Blog ili uweze kujifunza zaidi.
0 Comments