F Mkuu wa mkoa wa kusini Unguja awataka wtendaji kuwa wakarimu | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Mkuu wa mkoa wa kusini Unguja awataka wtendaji kuwa wakarimu

 Mkuu wa mkoa wa kusini Unguja awataka wtendaji kuwa wakarimu



Na Thabit Madai,Zanzibar.

MKUU wa Mkoa wa kusini Unguja, Rashid Hadid Rashid amewataka viongozi na watendaji wa mkoa huo kuwa na busara pamoja na hekima wakati wanapowahudumia wananchi ili kufikia malengo ya Serikali kutoa huduma zilizo bora kwa wananchi wake.


Akizungumza mara baada ya hafla maalum ya kumuapisha Katibu tawala wa mkoa Salum Kassim Ali aliyeteuliwa hivi karibuni na Rais wa Zanzibar Dk Hussein Ali Mwinyi ambapo hafla ya kumuapisha ilifanyika Tunguu atia ofisi za mkoa kusini Unguja.


Mkuu huyo wa Mkoa alisema kuwa,ifike wakati watendaji wa Serikali wawe  na busara pamoja na hekma wakati wakitoa huduma kwa wananchi kwa lengo kuboresha huduma kwa wananchi.


“Wananchi wanamatumaini makubwa na serikali hivyo kuna kila sababu ya kuwa na ukarimu kwa wananchi pindi wanapofika katika taasisi za serikali kwa lengo la kupata huduma,” alisema.


Aidha mkuu huyo wa mkoa amewataka viongozi na watendaji wa mkoa huo kuendeleza mashirikiano yaliyopo ili kuhakikisha wanatatua matatizo ya wananchi katika maeneo yao sambamba na kumtaka katibu tawala kutosikiliza maneno ya nje yasiyokuwa na manufaa na badala yake kuwajibika ipasavyo katika majukumu yake.


Kwa upande wake katibu tawala wa mkoa huo ndugu. Salum Kassim Ali amesema atahakikisha anatekeleza majukumu yake kikamilifu ili kuona kwamba mkoa huo unaimarika zaidi kimaendeleo.


Mara baada ya kufanya makabidhiano ya ofisi aliyekuwa katibu tawala wa mkoa huo Bi. Fatma Mohammed Juma amewashukuru viongozi na wafanyakazi wa mkoa huo kwa mashirikiano makubwa waliyompatia katika kipindi chote cha uongozi wake na kuahidi kumpa mashirikiano katibu tawala kwa wakati wote atakapomuhitaji.


 Katika hafla hiyo iliyoenda sambamba na makabidhioano ya ofisi baina ya katibu tawala mpya na katibu tawala aliemaliza muda wake.

Post a Comment

0 Comments