F Wananchi wakili kuharibu miundombinu. | Muungwana BLOG

Wananchi wakili kuharibu miundombinu.

 


Na Maridhia Ngemela.

Wanavijiji wa Kata ya Tabaruka na Kafundikile wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza wametakiwa kuacha kutumia mabomba ya maji kutengenezea bangiri za mikononi na miguuni kwa ajili ya urembo ili kuendelea kutunza miundo mbinu ambayo inawasaidia kwamanufaa yao.


 Mkuu wa Wilaya ya  Sengerma  Emmanuel Kipole amesema hayo wakati  wa  maadhimisho ya wiki ya maji na uwekaji jiwe la msingi katika mradi wa maji Tabaruka-Buswalangiri na mradi wa kituo cha kuchotea maji cha Mwaliga Nyamahona  mkoani Mwanza.


Kipole amesema wananchi hao wamekuwa  na tabia ya  kuharibu miundombinu ya maji kwa kuchukua mabomba yaliyotandikwa chini ya ardhi kwa ajili ya kupitishia maji na kutengenezea urembo huo.


"Miradi ya maji ilikuwepo tangu mwaka 1970 lakini mkakata kata mabomba na  kutengeneza mabangiri ya kuvaa mikononi na miguuni. Na bado tumeendelea kutumia teknolojia ileile hatujaleta mabomba ya chuma: ni mabomba yaleyale yatakayowafaa kutengeneza mabangiri,"amesema kipole na kuongeza


"Sasa kutengeneza bangiri uvae wewe au tupeleke maji kwenye jamii wewe mwenyewe utafakari,"


Amewataka wananchi wote wa Mkoa wa Mwanza kuwa walinzi wa miundombinu ya maji inayotekelezwa na serikali kwa gharama kubwa ili kuendelea kunufaika na lasilimali ya nchi.


Hata hivyo wananchi wamekiri kukata mabomba hayo kipindi cha nyuma kwa ajili ya kutengenezea mabangiri huku wakidai hawatokata tena kwakuwa mabangiri hayo yamepitwa na wakati.


Awali, Meneja wa Wakala wa maji safi na usafi wa mazingira vijijini (Ruwasa) mkoani humo, Immaculata Raphael amesema Ruwasa inatarajia kukamilisha miradi ya maji safi 17 mkoani Mwanza itakayogharimu Sh 8.2 bilioni ifikapo juni mwaka huu.


Amesema miradi hiyo itawanufaisha zaidi ya wananchi 57,000 kupitia vituo vya kuchotea majj 86.


"Kwa Wilaya ya Sengerema katika mwaka wa fedha 2021/22 tumepanga kujenga miradi mipya  ya maji saba lengo ni kuhakikisha mama abebi ndoo kichwani,"amesema Shange


Amesema, katika wiki hii ya maji inayoanza leo Machi 16 hadi machi 22 mwaka huu watazindua miradi ya maji, kuweka mawe ya msingi na kuwaelimisha wananchi juu ya haki na wajibu wake juu ya rasilimali ya maji.


Naye Meneja wa Ruwasa wilayani Sengerema Kassian Witike amesema mradi wa Tabaruka-Buswalangiri umegharimu Sh400 milioni huku mradi wa kituo cha kuchotea maji cha Mwaliga Nyamahona ukigharimu Sh700 milioni

Post a Comment

0 Comments