Na Timothy Itembe Mara.
MKUUwa wilaya Tarime mkoani Mara,Mtemi Msafiri ameagiza vibanda vya wafanyabiashara kuendelea kumilikiwa na waliovijenga hadi hapo mazungumzo yatakapofanyika baina ya wamiliki na mkurugenzi wa halmashauri ya Tarime Mjini.
Hatua hiyo imekuja baada ya wafanyabiashara wa vibanda kufika ofisini kwake kulalamikia kuwa halmashauri ya Mji wa Tarime inawanyang'anya wamiliki vibanda na kuwasainnisha mikataba wafanyabiashara kunyume cha utaratibu.
"Nimefuatilia ili kujua kama mna mkataba uliosainiowa baina ya wamiliki wa vibanda na halmashauri ya mji ila nikaona hakuna mkauataba uliopo bali kuna rasimu ya mkataba ambao unasema wamiliki watamiliki ambao ni wajenzi wake watatumia vibanda hivyo kutoka mwaka 2016 hadi 2031 huku halmashauri ikiwataka wamiliki hao kutumia kuanzia mwaka 2016 hadi 2026 ambapo wote kwa pamoja wameingia mgogoro mimi nasema mtaendelea kutumia vibanda vyenu hadi hapo mtakapom kaa chini na halmashauri ya mji na kukubaliana"alisema Msafiri.
Kwa hatua nyingine Msafiri aliwataka halmashauri kufungua vibanda vyote ambavyo vilikuwa vimefungwa na kuwataka kuendelea kutii maagizo anayoyatoa huku wakizingatia kuwa yeye nibosi wa wilaya siovinginevyo.
Mmoja wa wamiliki wa vibanda vya soko la RebuJunya Mwera alisema kuwa awali halmashauri hiyo iliwapa rasimu ya mkataba mwezi julai 2016 ambaye katika mkataba huu atajulukana kama mpangaji kwa upande mmoja.
Mwera alibainisha kuwa rasimu hiyo tafsiri ya maneno ya mkataba 1,mpangaji maana yake mmiliki wa kiwanja No 78 kitalu ''L'' kilichopo halmashauri ya mji na ndiye mwenye mamlaka ya kuweka mpangaji kwenye kibanda na kudai kodi kutoka kwa mpangaji huyo.
11,Mpangaji maana yake ni mtu anayefanyabiashara ndani ya kibanda husika kiwanja husika katika soko la Rebu ndani ya halmashauri ya mji wa Tarime na ndiye mjenzi wa kibanda.
111,Kibanda maana yake ni jengo au chumba cha biashara katika kiwanja No 78''kitalu L''ambapo aliendelea kuwa mara nyingi mkataba wowote ni kuleta mwaafaka na manufaa kwa pande zote husika lakini kwa halmashauri yetu mkataba
uliotayarishwa unatugandamiza.
Mwera aliongeza kusema wajenzi waliomba maeneo kadhaa kupatiwa ufumbuzi ikiwemo Kodi ya vibanda kuwa shilingi 10,000 na 15,000 kwa mwezi kulingana na hali halisi ya mazingira ya soko na mtaji.
mda wa wajenzi kumiliki vibanda kuwa miaka 15 au miaka 20, mkataba kuanza januari 2017 badala ya julai 2016 mapitiao ya mkataba kuwa kila baada ya miaka 3 badala ya mwaka mmoja .malipo ya kodi kufanyika kila baada ya miezi mitatu.
Naye Mariamu Maigga alisema kuwa baadhi ya wafanyabiashara wamefungiwa vibanda kinyume cha sheria ambapo wameshindwa kulipia watoto mahitaji ya shule kutokana na kushindwa kuifanyabiashara.