Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amekagua mradi wa maji Isimani-Kilolo unaotekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Iringa (Iruwasa) na kutoa mwezi mmoja kwa watendaji wa wizara yake kuhakikisha wananchi wa Isimani na Kilolo wanapata maji.
Ameeleza hayo kwenye ziara hiyo ya kukagua hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa mradi huo utakaohudumia vijiji vya Isimani na Kilolo mkoani humo.
Amempa maelekezo katibu mkuu wa wizara yake, Antony Sanga kupeleka Sh100 milioni kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa tanki la kuhifadhia lita 500,000 za maji linalojengwa katika mlima Ndiuka uliofikia asilimia 86.
Pia amemuelekeza mkurugenzi wa Iruwasa kukamilisha ujenzi wa tanki hilo ifikapo Juni 2021 ili wananchi wa Isimani na Kilolo waanze kupata huduma ya maji
