Rais wa Somalia aitisha uchaguzi katika harakati za kutuliza mvutano


Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Mohamed leo ameitisha uchaguzi na kutaka mazungumzo yafanyike baada ya hatua ya kurefushwa kwa muhula wake kwa miaka miwili kusababisha machafuko mabaya zaidi ya kisiasa kuwahi kushuhudiwa nchini humo kwa miaka kadhaa. 

Rais Abdullahi maarufu kama Farmajo amelihutubia taifa saa saba usiku wa kuamkia leo baada ya masaa kadhaa ya kusubiri hotuba yake. 

Taharuki ilikuwa imetanda katika mji wa Mogadishu wakati ambapo vikosi vya serikali na wanajeshi wanaounga mkono upinzani walikuwa wamejiweka tayari kwa mapambano huku raia wakiukimbia mji huo. 

Pande hizo hasimu zilishambuliana Jumapili iliyopita kufuatia mivutano ya muda mrefu iliyosababishwa na kucheleweshwa kwa uchaguzi uliokuwa umepangiwa kufanyika Februari na hatua ya Farmajo kuongeza uongozi wake mapema mwezi huu.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi