China yafuta upandaji wa mlima Everest


China imetangaza kuwa zoezi la kupanda mlima Everest katika msimu wa Spring umefutwa kutokana na janga la virusi vya corona.


Shirika la Habari la Xinhua lilitangaza kuwa China imeamua kufuta msimu wa kupanda kwa majira ya spring mwaka wa 2021 upande wa Tibet wa Mount Everest, kilele cha juu zaidi duniani.


Kauli hiyo ilitolewa na Utawala Mkuu wa Michezo wa China.


Nepal, ambayo ina uhaba wa mitungi ya oksijeni, imewataka wapandaji kurudisha mitungi yao mitupu.


Baada ya kufungwa kwa mwaka jana, 408 waliruhusiwa kupanda Everest msimu wa Aprili-Mei. Wapandaji 21 wa China waliidhinishwa kupanda mlima ho.

Post a Comment

0 Comments