Costech Yaahidi Kuboresha Na Kuendeleza Bunifu Za Makisatu

 


TUME ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) wamejipanga kuhakikisha bunifu zilizowasilishwa katika mashindano ya taifa ya ubunifu (MAKISATU) yaliyomalizika hivi karibuni jijini Dodoma zinaboreshwa na kuendelezwa.


Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa COSTECH,Dk Amosi Nungu kufuatia agizo la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa la kuzitaka taasisi zinazohusika na kuendeleza bunifu kuhakikisha zinasaidia kuboresha kazi zao na kuzifikisha sokoni.


Dk Nungu alisema kwamba taasisi yake kw akuangalia bunifu zilizowasilishwa wamejipanga kuhakikisha wanaziboresha ili waliobuni bunifu hizo wanapiga hatua na kuchangia pato la uchumi la taifa.


“Nimefurahi kuona mwaka huu wabunifu wamewasilisha vitu vikubwa sana katika MAKISATU hii inaonyesha jinsi gani wanavyoelewa pale wanapopewa marekebisho kwa ajili ya kuboresha kazi zao,”alisema Dk Nungu.


Dk Nungu alisema wao Kama wadau wakubwa wameridhika na mashindano hayo kutokana na kwamba wameona jinsi gani wabunifu walivyozingatia maboresho waliyopewa na kubuni kazi nzuri ambazo wengi wao wamepata ushindi wakati wa kilele cha kufunga kwa mashindano ya MAKISATU .


“ Tumefurahi kuona mashindano hayo ambayo hata Waziri Mkuu ameshuhudia na kukubali kuwa Tanzania kuna watu wana vipaji na wenye bunifu nzuri za kisayansi “, alisema Dk Nungu.


Alisema COSTECH imefarijika sana kuona wabunifu mwaka huu wamekuja na vitu vikubwa vya kitaalamu ambavyo kama vikipata uendelezaji vitakuwa na tija katika Taifa.


Katika Hotuba yake ya kufunga maonesho hayo,Waziri Mkuu alitoa maagizo kwa COSTECH, SIDO, VETA na Don Bosco kuhakikisha wanakuwa karibu na wabunifu hao kwa kuwaendeleza katika mawazo yao ya ubunifu ikiwemo kuziendeleza bunifu zao.


Waziri Mkuu alisema Taasisi hizo ndio zimepewa dhamana na Serikali kuhakikisha wabunifu hao wanaendelezwa na kukua ili Bunifu hizo ziwe na tija katika Taifa.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items