Wimbi la pili la Covid-19 lasambaa maeneo ya vijijini ya India

 


India leo imeripoti maambukizi mapya zaidi ya laki tatu ya Covid-19 ndani ya kipindi cha saa 24 na vifo 4,000, katikati mwa ongezeko la wasiwasi juu ya kuenea kwa maradhi hayo katika maeneo ya vijijini, ambako hakuna huduma za kutosha kukabiliana na janga hilo. 


Wimbi la pili la maambukizi ya Covid-19 limekuwa likisambaa katika miji mingi ya India tangu mwezi uliopita na kudhoofisha miundombinu ya afya, ikiwa ni pamoja na hospitali na maeneo ya kuchoma maiti kuzidiwa. 


Ripoti za hivi karibuni za idadi kubwa ya watu wa vijijini kuumwa na kugunduliwa kwa miili iliyotelekezwa kando ya mito au kuzikwa mchangani, zinaashiria kuwa ugonjwa huo umeenea katika maeneo ya vijijini. Serikali ya shirikisho tayari imetoa mwongozo kwa serikali za majimbo wa namna ya kukabiliana na maradhi hayo.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items