F Fahamu namna za kujitibu tatizo la kuvimba miguu kwa mama mjamzito | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Fahamu namna za kujitibu tatizo la kuvimba miguu kwa mama mjamzito

 

Kuuma na kuvimba kwa miguu wakati wa ujauzito ni tatizo ambalo hujitokeza kwa wanawake wengi. Hili tatizo likitokea hasa hasa miezi ya mwisho wa ujauzito, husababishwa na kutokuwa na calcium na chumvi ya kutosha mwilini, pialinaweza jitokeza kama damu inashindwa kuzunguka vizuri mwilini.   


  • Jinsi ya kupunguza au kuzuia hili tatizo. 
  • Jaribu kufanya mazoezi ya kutembea, kuogelea kadri ya uwezo wako.
  •  Jaribu kufanya mazoezi ya kunyoosha misuli kama ya Yoga.
  • Jaribu kupata massage ya mwili mzima angalau mara moja kwa mwezi.
  •  Fanya mazoezi ya pelvic rocking kusaidia mzunguko mzuri wa damu, chuchumaa mara kwa mara, kaa style ya kihindi/ tailor sitting, lala na miguu ikiwa imeegeshwa juu ya mito. Mazoezi haya yote tulishaiongelea jinsi ya kuifanya kwenye maada ya mazoezi maalum kwa ujauzito pia jinsi ya kulala ili kuhakikisha damu huzunguka vizuri.
  • Hakikisha unapata calicum na chumvi ya kutosha katika diet yako. 

Post a Comment

0 Comments