Kansela Merkel azungumza na Netanyahu kuhusu machafuko ya Mashariki ya Kati

 


Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amezungumza na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kuhusu machafuko yanayoendelea Mashariki ya Kati na kutilia msisitizo kujitolea kwa Ujerumani kusimama na Israel na pia haki ya Israel kujilinda.

Merkel ameshutumu muendelezo wa ufyatuliaji makombora kutoka Gaza kuelekea Israel, na kuelezea matumaini yake kwamba mgogoro huo utamalizika haraka iwezekanavyo ili kuepusha maafa zaidi baina ya pande zote mbili. 

Kwingineko, Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amemwambia kiongozi mkuu wa Kanisa Katoliki ulimwenguni, Papa Francis, kwamba jumuiya ya kimataifa inapaswa kuiwekea Israel vikwazo kufuatia mashambulizi yake dhidi ya Wapalestina. 

Ofisi ya Erdogan imesema viongozi hao walizungumza kwa njia ya simu na kwamba Erdogan amemtaka Papa Francis kuendelea kuzungumzia mashambulizi hayo. Hapo jana, Papa Francis alisema ongezeko la idadi ya vifo ni suala lisilokubalika.


Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi