Makombora ya Israel yaporomosha jengo la mashirika ya habari, Gaza


Shambulizi la anga lililofanywa na Israel kwenye Ukanda wa Gaza limeharibu na kuliporomosha jengo moja la ghorofa 12 lenye ofisi kadhaa za mashirika ya habari. 


Tukio hilo linatajwa kuwa hatua ya karibuni kabisa ya jeshi la Israel kujaribu kuzima kazi ya kuripoti yanayoendelea kwenye Ukanda wa Gaza wakati ikiendelea kupambana na wanamgambo wa Hamas. Shambulizi hilo limetokea kiasi saa moja baada ya jeshi la Israel kuamuru watu kulihama jengo hilo ambalo lilikuwa ni ofisi ya shirika la habari la Associated Press, kituo cha televisheni cha Al-Jazeera na ofisi nyingine pamoja na makaazi. 


Hakuna maelezo yaliyotolewa kuhusu kwanini Israel imelilenga jengo hilo. Hayo yamejiri saa chache tangu ndege za Israel zilipofanya hujuma kwenye kambi yenye idadi kubwa ya wakimbizi- kwenye mji wa Gaza na kuwauwa wapalestina 10 wengi wakiwa watoto. Kila upande kwenye mapigano hayo unajaribu kutumia nafasi inayopatikana kufanya mashambulizi wakati juhudi za kutaka kusitishwa mapigano zikiendelea.

Post a Comment

0 Comments