F Tetesi za soka Ulaya leo 23/05/2021 | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Tetesi za soka Ulaya leo 23/05/2021

Chelsea wamerejesha shauku yao kwa mchezaji wa West Ham Declan Rice na wanaweza kumtumia mshambuliaji Tammy Abraham, 26, kama sehemu ya mpango wa kubadilishana. Manchester United na Manchester City wanavutiwa kumsajili Rice. (Sunday Telegraph - subscription required)


Manchester City ilikuwa na zabuni ya mshambuliaji wa Tottenham na England Harry Kane, 27, aliyekataliwa na mwenyekiti wa Spurs, Daniel Levy wakati wa usajili wa Januari. (Sunday Mirror)

Manchester United wako tayari kuweka mezani ofa kubwa ya kumpeleka Kane Old Trafford. Ofa ya United itamlipa Kane fidia kwa mapato yoyote yaliyopotea huko Spurs(Sunday Times - subscription required)


Wachezaji wa United na wachezaji wengine wa England Marcus Rashford, Luke Shaw na Harry Maguire wanatarajia kumshawishi Kane ajiunge na kilabu hicho.(Sun on Sunday)


Kiungo wa Guinea Naby Keita, 26, anataka kuondoka Liverpool na wakala wake amewasiliana na Atletico Madrid kupima uwezekano wa kuhamia kwa mabingwa wapya wa Uhispania.(AS - in Spanish)


Everton na Juventus wana nia ya kumsajili mlinda mlango wa Argentina mwenye umri wa miaka 34 Sergio Romero, ambaye anatamani kuondoka Old Trafford baada ya 'kupuuzwa' na Ole Gunnar Solskjaer msimu huu.(Mail on Sunday)


Manchester United wanajiandaa kumnunua winga wa Bayern Munich mwenye umri wa miaka 24 Kingsley Coman. (Bild - in German)


Mshambuliaji wa Crystal Palace na Ivory Coast, Wifried Zaha,28, amesena ikiwa ''timu ya juu'' itataka kumsajili, hatakataa. Amekuwa akihushwa na Arsenal na Everton (The Face)


Mshambuliaji wa Kiingereza wa miaka 25 wa Middlesbrough Ashley Fletcher amekubali kujiunga na Watford kwa mkataba wa miaka mitano atakapokuwa huru mwezi Juni. (Sun on Sunday)


Wakati huo huo, Crystal Palace imeonesha nia ya uhamisho wa mchezaji wa FC Copenhagen na Denmark, Victor Nelsson, 22, ambaye hapo awali alikuwa akihusishwa na Aston Villa.(Mail on Sunday)


Leicester City ndio kilabu cha hivi karibuni kujiunga katika mbio za kumnasa beki wa Southampton na England Ryan Bertrand, na Arsenal na AC Milan pia wanahusishwa na beki huyo wa kushoto wa miaka 31, ambaye mkataba wake unamalizika msimu huu wa joto.(Talksport)


Wakala wa mshambuliaji wa Inter Milan na Argentina Lautaro Martinez, 23, amekutana na Atletico Madrid na Real Madrid.(Marca)


Kiungo wa kati wa Brazil Fernandinho, 36, yuko tayari kuongeza muda wake wa kucheza na Manchester City kwa kusaini mkataba mpya wa mwaka mmoja. (Sunday Times - subscription required)


Kiungo wa Ureno Bruno Fernandes, 26, anakaribia kukubali mkataba mpya wa Pauni 200,000 kwa wiki na Manchester United.(Sunday Mirror)



Juventus inaweza kuhamia kwa mshambuliaji wa Barcelona, ​​30, Antoine Griezmann kama mbadala wa mshambuliaji wa Ureno Cristiano Ronaldo, 36, ambaye hatma yake bado iko mashakani. Juve wanafikiria uhamisho wa mkopo kwa mshambuliaji huyo wa Ufaransa, lakini pia wako wazi kwa kubadilishana na mshambuliaji wa Argentina Paulo Dybala, 27.(La Stampa - in Italian)


Newcastle United itajaribu tena kumsajili kiungo wa Leicester City Hamza Choudhury, 23, baada ya kumkosa mchezaji huyo wa zamani wa England chini ya miaka 21 mwezi Januari.(Mail on Sunday)


Kocha wa Roma ajaye , Jose Mourinho ana nia ya kumsajili mshambuliaji wa Uholanzi Wout Weghorst mwenye umri wa miaka 28 kutoka Wolfsburg kama mbadala wa mshambuliaji wa Bosnia Edin Dzeko, 35.(Gazzetta dello Sport - in Italian)


Crystal Palace na West Ham wanaongoza mbio za kumuwania kiungo wa kati wa England mwenye umri wa miaka 22, Josh Hawkes, ambaye pia amekuwa akihusishwa na Newcastle United na Leeds United.(Team Talk)

 

Post a Comment

0 Comments