Watu 30 wahukumiwa kifo DRC


Watu 30 wamehukumiwa adhabu ya kifo nchini Jamhuri ya Kidemkrasia ya Congo, baada ya shauri lililoendeshwa kwa siku moja kuhusiana na kushiriki kwao katika vurugu dhidi ya polisi wakati wa sherehe za sikukuu ya Iddi mjini Kinshasa. 


Wakili wa vyama vya kiraia Chief Tshipamba ameliambia shirika la habari la AFP kuwa watu hao 30 wamehukumiwa kifo katika shauri lililoanza jana Ijumaa siku moja baada ya kutokea kwa machafuko hayo. 


Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo haijawahi kutoa hukumu ya kifo tangu sheria ya kutoa hukumu hiyo ilipositishwa mwaka 2003, tangu wakati huo hukumu hizo hubadilishwa kuwa kifungo cha maisha jela.

Post a Comment

0 Comments