Fufu lililopasuka na taya vilipatikana karibu na Ramla nchini IsraelImage caption: Fufu lililopasuka na taya vilipatikana karibu na Ramla nchini Israel
Watafiti wanaofanyia kazi nchini Israeli wamebaini aina mpya ya mtualiyeishi zamani ambaye aliishi karibu na viumbe wetu kwa zaidi ya miaka 100,000.
Wanaamini kwamba mabaki yaliyogunduliwa karibu na mji wa Ramla yanawakilisha moja ya kikundi‘’cha mwisho ‘’cha binadamu wa kale zaidi.
Mabaki yaliyopatikana ni pamoja na sehemu ya fuvu na taya vya mtu aliyeishi kati ya miaka 140,000 na 120,000 iliyopita.
Maelezo ya uvumbuzi huo yamechapishwa katika jarida la kisayansi .
Watafiti hao wanadhani kwamba mtu huyo alitokana na spichi wa zamani ambao walisambaa kwenye eneo hilo, maelfu ya miaka iliyopita na kuongezeka kwa binadamu wa kale (Neanderthals) barani Ulaya na wenzao wanaofanana katika bara Asia.
Wanasayansi wameita uvumbuzi wao mpya jina la "Nesher Ramla Homo type".
Dkt Hila May wa Chuo Kikuu cha Tel Aviv amesema uvumbuzi huo unabadilisha hadithi ya mabadiliko ya binadamu hususan wale wa kale.
Picha ya jumla ya mabadiliko ya binadamu wa kale miaka ya nyuma walihusishwa na karibu na Ulaya.
''Yote ilianzia katika Israel. Tunasema kwamba kikundi cha wakazi kilikua chanzo cha idadi ya watu," aliiambia BBC News.
