Kuna wagonjwa wa corona ambao wameshaonekana nchini kwenye wimbi la tatu-Rais Samia

 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema tayari kuna wagonjwa wa corona ambao wameshaonekana nchini kwenye wimbi la tatu, amewataka viongozi wa dini kuwaeleza waumini kuchukua tahadhari

“Duniani kuna wimbi la tatu la Corona, ishara ndani ya Nchi tayari zinaonekana, tayari tuna wagonjwa ambao wameshaonekana kwenye wimbi hili la tatu,"

"Nilitembelea Hospitali ya Mwananyamala, kuna wodi daktari mfawidhi alikuwa ananiingiza akaniambia humu kuna wagonjwa wenye matatizo ya kupumua. Nikwambia kuwa muwazi, ni COVID[19] kasema, ndio, COVID. Nikawaambia wapigapicha wangu tokeni haraka,"

"Kwa hiyo ni kusema hili jambo bado lipo, tusijiachie, tuchukue Tahadhari zote na tunawaomba sana viongozi wa dini mliseme hili kwa sauti kubwa kwa waumini wetu ili tujiepushe na vile vifo vya makundi,"- Rais Samia Suluhu Hassan


Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items