WHO: Afrika iko katika wimbi la tatu la maambukizi ya Covid-19


Afrika inakabiliwa na wimbi la tatu la coronana kuna haja ya kupatatikana nkwa chanjo zaidi, Shirika la Afya Duniani (WHO)limesema.

Idadi ya watu walioambukizwa virusi vya corona imepita milioni tanohuku nchi saba zikiishiwa na chanjo.

"Africa inahitaji mamilioni zaidi ya chanjo kwa sasa," Mkurugenzi wa WHO wa kanda Afrika Matshidiso Moeti amesema.

Afrika Kusini, Morocco, Tunisia, Ethiopia na Misri zimerekodi viwango vya juu zaidi vya maambukizi ya corona barani humo.

Uganda na Namibia zinakabiliwa na wimbi la tatu la maaambukizi huku makumi ya watu wakiripotiwa kufa kila siku.

Jumla ya watu elfu136,030 wamefariki kutokana na ugonjwa wa Covid -19 katika nchi tofautiza Afrika, kulingana na WHO.

Kirusi cha Delta kimegunduliwa katika nchi 14 za Afrika huku kirusi cha Beta, kilichogunduliwa mara ya kwanza Afrka Kusini , kikifikakatika nchi 25.

WHO inasema hakuna muda kamili ulitowa kubaini ni lini chanjo zaidi zitapatikana lakini limesistiza kwamba kuna haja kushughulikia upatikanaji wake kwa dharura.

Post a Comment

0 Comments