Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson ametangaza mipango ya kuondoa makatazo mengi vya kujikinga na Virusi vya corona ikiwa ni pamoja na kuvaa barakoa, kukaa au kusimama umbali wa mita kadhaa (social distancing) kuanzia Julai 19, akihimiza uwajibikaji wa mtu binafsi katika kujikinga badala ya amri ya serikali.
Hapo awali Johnson alikuwa na lengo la kuondoa vizuizi hivyo mnamo Juni 21, lakini alilazimika kurudisha tarehe hiyo kwa sababu ya kuongezeka maambukizi ya virusi vya Corona aina ya delta
Aina hiyo mpya ya virusi ilichangia kuongezeka kwa maambukizi yote mapya ya Covid-19 huko Uingereza, na kusababisha wasiwasi miongoni mwa wananchi.
Lakini uchomaji wa chanjo nyingi umesaidia kupunguza watu kulazwa hospitalini na vifo.
0 Comments