Waangalizi Sudan Kusini wahofia kuvunjika kwa mkataba wa amani


Waangalizi wa kimataifa nchini Sudani Kusini wamesema kuwa wana wasiwasi kuhusu mapigano yanayoendelea kutishia utekelezaji wa makubaliano ya amani.

Mapigano yanaripotiwa katika sehemu tofauti za nchi hiyo kati ya vikosi vya serikali na vikundi tofauti vya wapinzani.

Wachunguzi hao wa kusitisha mapigano wanasema wamekuwa wakirekodi mapigano katika jimbo la Central Equatoria inayodaiwa kuhusisha vikosi vya serikali na waasi National Salvation Front (NAS).

Kumekuwa na mashambulizi makali katika vituo tofauti yaliyoripotiwa katika jimbo la Upper Nile na Central Equatorial ambako vikosi vimekuwa vikipata mafunzo.

Waangalizi wametaka uongozi wa jumuiya ya IGAD kuitaka Sudani Kusini kuchukua hatua za haraka ‘’kuzuia kusambaratishwa kwa makambi ya mafunzo na kuundwa kwa jeshi la kitaifa la umoja".

Mwezi Aprili, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilionya kuhusu hatari ya kurudi kwenye mzozo mkubwa huko Sudan Kusini, kwa sababu ya kutekelezwa polepole kwa makubaliano ya amani.

Rais Salva Kiir na mpinzani wake mkuu wa zamani, Riek Machar, sasa Makamu wa Kwanza wa Rais, walitia saini makubaliano ya amani mnamo Septemba 2018 - lakini ukosefu wa usalama bado umekithiri nchini.

 

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items