Wahamiaji 57 wafa maji katika pwani ya Libya

Takribani watu 57 wanaripotiwa kuzama katika pwani ya Libya – katika tukio la hivi punde la idadi kubwa ya maafa ya wahamiaji wanaojaribu kufika Ulaya.

Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Uhamiaji nchini Libya, Federico Soda, alisema alikuwa na hofu.

IOM ilisema manusura waliwaambia wafanyikazi wake kuwa wanawake 20 na watoto wawili walikuwa miongoni mwa wale waliokufa.

Chanzo cha ajali hiyo karibu na bandari ya Khoms ya Libya hakijulikani.

Boti zinazoondoka Libya kwenda Ulaya kawaida huwabeba watu wengi kupindukia na kuanza safari usiku ili kukwepa kugunduliwa na walinzi wa pwani.

Hali ya hewa iliyoboreka imechangia kuongezeka kwa idadi ya boti zinazojaribu kuvuka bahari ya Mediterania kutoka Afrika Kaskazini.

Inakadiriwa watu 1,100 wamekufa hadi sasa mwaka huu, zaidi ya mara mbili ya idadi ya waliofariki kipindi kama hiki mwaka jana.

Post a Comment

0 Comments