Waziri Ummy Mwalimu atoa siku saba uchunguza vifo vya wanafunzi tatu


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais ,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Ummy Mwalimu ametoa siku saba kwa vyombo vya ulinzi na usalama kuchunguza vifo vya wanafunzi tatu waliofariki kwa kufunikwa na kifusi katika shule ya msingi Mbori, Kata ya Motondo wilayani Mpwapwa.

Wakati huo huo Ummy amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kuwaondoa Walimu wote wa shule ya Msingi Mbori kupisha uchunguzi unaondelea.

Waziri Ummy ametoa kauli hiyo wakati aliposhiriki kuaga Miili ya wanafunzi tatu waliofariki kwenye ajali ya kufukiwa na mchanga katika shule ya Msingi Mbori Julai 27, mwaka huu.

Post a Comment

0 Comments