Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken leo atakutana na viongozi wa India akiwa katika ziara yake ya kwanza nchini humo kama mwanadiplomasia wa ngazi ya juu.
Maafisa wa India wanatarajia
kuzungumzia wasiwasi wao juu ya kujiimarisha kwa wanamgambo wa kundi la
Taliban nchini Afghanistan pamoja na kuishinikiza Marekani kuiunga mkono
zaidi India dhidi ya China.
Kwa upande wake waziri huyo wa mambo ya nje
wa Marekani anatarajiwa kuzungumzia wasiwasi uliopo juu ya haki za
binadamu wakati atakapokutana na waziri mkuu wa India Narendra Modi na
waziri mwenzake wa mambo ya nje Subrahmanyam Jaishankar.
Uhusiano wa
Marekani na India kihistoria umekuwa wa misukosuko lakini suala la China
kuzidi kujiingiza katika mgogoro na India kumeifanya Marekani na India
kuwa karibu na hasa tangu mapigano makali yaliyosababisha umwagikaji
damu mwaka jana katika mgogoro wa eneo la mpaka baina ya India na China
la Himalaya. India ni sehemu ya ushirikiano na Marekani,Japan na
Australia dhidi ya China.
Ingawa kuna hisia kwamba uungaji mkono wa
Marekani kwa India chini ya utawala wa rais Joe Biden sio mkubwa kama
ilivyokuwa chini ya Donald Trump ambaye maafisa wake waliikosoa waziwazi
China na kuiunga mkono India katika mgogoro wake na China.
