Jambo la msingi la kuzingatia wakati wa kutangaza biashara katika mitandao ya kijamii

Miongoni mwa njia ambazo zinakua kwa kasi  sana kwa hivi sasa katika suala la kutangaza biashara ni pamoja na kutumia mitandao ya kijamii ( social networks).  Ipo mitandao mbalimbali ya kijamii  kama vile whatsapp, facebook, instagram na mengineyo mingi.

Njia hii ni nzuri na yenye kuvuta wateja wengi endapo mfanyabiashara huyo ataelewa namna ya kuvuta wateja wengi kwa kutumia njia hii. Njia hii ni rahisi na yenye kuwavuta wateja wengi kutoka sehemu tofauti tofauti.

Pamoja na kuwapo kwa mitandao hii  ya kijamii wengi wao wemekuwa wanatangaza pasipo kujua namna ya kutangaza na kitendo hiki kinawafanya watu hao wakose wateja huku wakizidi kutangaza biashara zao katika mitandao.

Binafsi nimekuwa nikiona watu  wakitangaza bishara zao huku wakisema nauza kitu fulani kwa maelezo zaidi  naomba unifuate inbox au tuwasiliane kwa namba hizi. Kwa kusema hivyo nakumbia huwezi kupata wateja wengi kwa sababu kuna mahali unakosea sana katika kutangaza biashara hiyo.

Unachotakiwa kufanya;
Ili uweze kuwapata wateja wengi kwa kupitia mitandao ya kijamii unatakiwa kueleza faida za bidhaa atakazozipata mteja pindi atakaponunua bidhaa husika.

Naomba nirudie tena kwa kusema "ili Ili uweze kuwapata wateja wengi kwa kupitia mitandao ya kijamii unatakiwa kueleza faida  atakazozipata mteja pindi atakaponunua bidhaa husika.

Kwa mfano kama wewe unafanya biashara ya kuuza simu, unaweza kusema Jipatie simu aina fulani kwa bei ya nafuu.

Mara baaada ya kusema hayo sasa unaongeza na faida zinazopatikana katika simu hiyo, kwa mfano unaweza kusema, simu hii ina uwezo mkubwa wa kukaa na chaji kwa muda mrefu, uwezo  wake wa internet ni ya kasi zaidi, Pia uwezo wake wa kuoinga picha ni wa kiwango cha hali ya juu zaidi.

Pia tunatoa warranty yake ambayo ni mwaka mmoja na miezi mitatu, kwa kufanya hivyo utamfanya mteja anayesoma tangazo hilo avutike na biashara unayouza/ kuifanya.

Kitendo cha kusema nauza simu fulani kwa maelezo zaidi wasiliana nami ni sawa na kumwambia mteja asije hii ni kwa sababu utakuwa hujamvutia kwa kitu chochote.

Kila wakati mteja huwa ananua bidhaa fulani ili kuweza kutatua matatizo au changamoto zinazomkabili hivyo ukiweza kumteka mteja kwa kumpa suluhisho la tatizo ambalo linamkuba utamfanya mteja huyo afutiwe na wewe mwisho atakuwa umemfanya kuwa mteja wako.

Hilo ndilo jambo la msingi analopaswa kulizingatia hasa pale unapokuwa unatengaza biashara yako kwa kutumia mitandao ya kijamii.

 

Post a Comment

0 Comments