Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi imeanza kupokea ushahidi kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Ramadhani Kingai katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu.
Kamanda
wa polisi ni miongoni mwa mashahidi katika keshi hiyo, mashahidi
wengine ni pamoja na aliyekuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya
Jinai (DCI), Robert Boaz.
Wengine
ni maofisa wa polisi kutoka makao makuu ya jeshi hilo vitengo vya
makosa ya kimtandao, uchunguzi wa silaha na uchunguzi wa maandishi na
wengine kutoka mikoani.
Mashahidi wengine ni maaskari kutoka
Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), akiwamo Luteni Denis Leo Urio kutoka
Kikosi cha Jeshi cha Makomandoo, 92 KJ Ngerengere, mkoani Morogoro.
Pia wamo maofisa wa sheria kutoka kampuni za huduma za simu za mkononi za Mic Tanzania Ltd (Tigo) na Aritel.
