Maafisa wa watatu wa zamani wa ujasusi nchini Marekani wamekiri kuipa nchi ya Falme za Kiarabu teknolojia ya udukuzi.
Maafisa hao wamekubali
pia kulipa karibu dola milioni 1.7 kutatua mashtaka ya uhalifu dhidi yao
katika makubaliano ambayo wizara ya haki Marekani imeyaelezea kama ya
kwanza ya aina yake.
Maafisa hao Marc Baier, Ryan Adams na Daniel
Gericke wanatuhumiwa kufanya kazi kama mameneja wakuu katika kampuni
moja iliyo na makao yake Falme za Kiarabu, iliyokuwa inafanya shughuli
za udukuzi kwa niaba ya serikali.
Waendesha mashtaka wanasema, watu hao
walipeana teknolojia ya udukuzi na mifumo ya kijasusi ya kukusanya
taarifa ambayo ilitumika kudukua kompyuta Marekani na nchi zengine
duniani.
