Na Andrew Chale
MTANZANIA
mwenye asili ya Zanzibar Muslim Nassor maarufu kama Jazzphaa Jazz
anayefanya shughuli zake nchini Ujerumani amechaguliwa kuwa mmoja wa
watakaokuwa kwenye tamasha kubwa la Kimataifa la filamu za Afrika,
zitakazofanyika Koloni, Ujerumani.
Kwa mujibu wa Jazz, Tamasha hilo linatarajiwa kufanyika siku ya Alhamisi tarehe 16 - 26 September mwaka huu.
"Ninayo
furaha ya kuwatangazia nimepata kuchaguliwa kuwa mmoja wa watu ambao
watatambulisha filamu na kuongoza maongezi ya filamu Kimataifa katika
tamasha la Filamu za Afrika hapa nchini Ujerumani Koloni." Alieleza
Jazzphaa.
Ambapo alibainisha kuwa, filamu 97 kutoka nchi 25 za Afrika zinatarajiwa kuoneshwa kwenye tamasha hilo.
Ikumbukwe
kuwa, Mwaka 2016 mtengenezaji wa Filamu kutoka Tanzania Amil Shivji pia
alipata nafasi ya kuchaguliwa kuonyesha Filamu yake ya Aisha.
Aidha,
Jazzphaa aliwashukuru wadau wote kwa ushirikiano katika harakati zake
mbalimbali ikiwemo ya kuongoza shughuli kwenye matamasha makubwa ya
Kimataifa ikiwemo tamasha la Kimataifa la Filamu la nchi za Majahazi
(ZIFF), Tamasha la Muziki la Sauti za Busara na mengine mengi pindi
awapo Visiwani Zanzibar, Tanzania.
"Safari inaendelea. Asanteni wote mlionifanya kuwa na nguvu ya kuamini ninacho kifanya." Alimalizia Jazzphaa.
Tamasha
hilo kwa mwaka huu ni la msimu wa 18 ambapo kila mwaka kimekuwa
likipokea filamu mbalimbali kutoka Mataifa yote ya Afrika ambapo majaji
uchagua zilizo bora na kuzipitisha.
