Huenda umewahi kusikua kuwa kuhusu watu wanaotumia pesa nyingi sana kugarimia maisha ya mbwa wao.
Lakini mara hii mambo sio mbwa tena. Mwanamke mmoja kwa jina amekuwa akitumia kitita cha Pauni4,000 kila mwaka kuwapendezesha njiwa wake wawili aliowaasili ambao kwa sasa wana chumba , kabati lao la nguo na hata kutembezwa ndani ya baiskeli ya watoto wachanga.
Meggy Johnson, mwenye umri wa miaka 23, kutoka Lincolnshire, aliwanusuru ndege hao aina ya njiwa kwa majina Sky na Moose, baada ya kupatikana wakiwa wametupwa walipokuwa bado vifaranga.
Bi Meggy Johnson aliwatunza na kuhakikisha kuwa wanarejea katika hali nzuri ya afya kwa kuwalisha kwa mikono yake kwa kipindi cha wiki sita- na katika kipindi hiki alitokea kujenga uhusiano wa karibu nao na kuwapenda sana.
Kwa sasa, njiwa hao wanaishi “maisha ya anasa” huku wakifanyiwa sherehe za siku ya kuzaliwa, wakipewa wanasesele laini na kutembezwa.
Licha ya huduma yake ya upendo, Meggy, mara nyingi hupata kauli za matusi kutoka kwa watu wasiojulikana ambao humuita“panya wa kuruka ”,lakini anasema ni marafiki zake wazuri na “wanastahili fursa”, ya kupewa matunzo bora.
Mpenzi huyu wa wanyama hutumia pauni 400 kila mwezi kuwafurahisha njiwa hao pamoja na ndege wengine wawili aliowaokoa.


