Zaidi ya madawati 300 yamekabidhiwa wilaya ya Nyamagana kuweza kupunguza changamoto


Na Maridhia Ngemela, Mwanza.

Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza Amina Makilagi amewaomba wadau mbalimbali kujitokeza zaidi kumsaidia changamoto za uhaba wa madawati na vyumba vya madarasa kama inavyofanya 

taasisi isiyo ya kiserikali ya Th Desk & Chair Foundation  kwa kuonyesha upendo kwa kutoa misaada mbalimbali ya kijamii.

Hayo aliyasema jana wakati akipokea msaada wa madawati 348 yaliyotolewa na taasisi hiyo kwa lengo la kupunguza changamoto ya upungufu wa madawati kwenye shule mbalimbali.

Alisema ni vema taasisi na makampuni kuiga mfano kutoka The Desk & Chair Foundation kwa sababu inatambua umuhimu wa kusaidia jamii katika masuala mbalimbali ikiwamo kuwakatia bima za afya watu wenye mazingira magumu, kutoa taa za sola kwa wanafunzi,kufunga taa za sola kwenye nyumba za nyasi vijijini 420, kugawa baiskeli 600 kwa watu wenye ulemavu, kujenga madarasa.

"Taasisi hii imekuwa msaada mkubwa kwa jamii kwa sababu imefanya mambo mengi ambayo hatuwezi kuyasema yote maana muda hautoshi kuyaelezea yote.

Hata hivyo amewataka wananchi ambao walipewa fedha za mkopo wa bila riba na taasisi hiyo kuwa waaminifu kwa kurejesha  ili na wengine waweze kunufaika na mradi huo sanjari na kuwataka walio nufaika na mradi huo kutoa mrejesho kwani huo ni uungwa ili taasisi hiyo iweze kutambua.


Mwenyekiti wa taasisi hiyo Sibtain Meghjee amesema madawati hayo yamefadhiliwa na familia mbili wazaliwa wa Mwanza wanaoishi Uingereza na Canada ambao ni familia ya marehemu Mzee G.B Damji imekuwa ikifadhili mambo mengi haswa kwenye elimu kwani siku za nyuma walijenga madarasa,vyoo na kutengeneza madawati Kibara mkoani Mara ambako waliishi kama Meneja wajenery ya Kibaha.

"Familia ya marehemu Andani ambayo ilikuwa ikiishi Malampaka ndiyo walifadhili madawati 200 kati ya haya 348 ya leo.

"Tunaomba madawati 50 ukabidhi kwa shule ya msingi Holy Face la jimbo kuu la katoliki Dodoma na madawati 40 tulikabidhi siku ya mwenge kwenye shule ya Bulale na madawati 25 tunakabidhi leo kwa madrasati Fisabillilahi iliyopo wilayani Ilemela na yaliyobaki tunakukabidhi mkuu wa Wilaya ili uweze kupeleka kwenye shule mbalimbali zenye uhiitaji ya huduma hii.

Aliongeza kuwa mwaka 2020/2021 taasisi hiyo imesaidia wanafunzi zaidi ya 10000 washule za msingi na sekondari wa elimu maalum na elimu ya juu kwa kutoa vifaa mbalimbali ikiwamo vitabu,madaftari,rim,kaluleta, sare za shule.

"Hadi hivi sasa tumeweza kufadhili zaidi ya wanafunzi 300 wa masomo ya vyuo vikuu na kozii maalum takribani kwa asilimia 40 ya wanafunzi kwani wamemaliza masomo yao na kuanza kulitumikia jamii.

"Taasisi hiyo imefadhili ujenzi wa madarasa 12 yaliyoharibika kwenye shule mbalimbali za msingi yakiwamo.madarasa mawili ya wanafunzi wenye mahitaji maalum ambayo yanakuwa na madawati, vyoo, jiko na bafu.

"Tumefanikiwa kufadhili madawati zaidi ya 4000 kwenye shule za msingi na sekondari za kanda ya ziwa na visiwani lengo ni kuhakikisha wanafunzi wanasoma kwenye mazingira bora.

Hata hivyo alisema taasisi hiyo ilianzisha mradi wa kukopesha mitaji midogo midogo ya bila riba kwa wanafunzi wa elimu ya juu na baadhi ya watu kukataa kurejesha mara baada ya kukopa na kupelekea kufeli kwa sababu ya wakopeshwaji kutorudisha mikopo hiyo kwani kitengo hicho kufungwa rasmi.

Alisema taasisi hiyo inakabiliwa na changamoto ya maombi mengi kutoka kwenye idara mbalimbali kwa upande wa elimu na wagongwa.

 

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items