Zaidi ya viongozi 100 kwenda New-York kushiriki mkutano wa baraza kuu la UN

 


Zaidi ya viongozi wakuu 100 wa nchi na serikali wanapanga kuhudhuria mkutano wa kila mwaka wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa wiki ijayo. 

Viongozi hao wakiwemo rais wa Marekani Joe Biden,mfalme Abdullah wa pili wa Jordan na marais wa Brazil na Venezuela watakuwepo New-York kushiriki mkutano huo kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa ya watakaozungumza kwenye baraza hilo.

Aidha viongozi wengine watakashiriki moja kwa moja mkutano huo ni mawaziri wakuu wa Japan,India na Uingereza pamoja na waziri mkuu Naftali Bennett wa Israel na rais wa mamlaka ya Wapalestina Mahmoud Abbas watakaotoa hotuba zao mbele ya hadhara hiyo.

Wanadiplomasia na viongozi wengi wamelalamika hadharani kwamba mikutano kwa njia ya vidio haiwezi kuwa sawa na mikutano ya ana kwa ana katika masuala ya kukabiliana na changamoto za kikanda na kidunia pamoja na mizozo.


Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items