Shahidi aliyepangiwa kusimama kusimama katika kesi ya Netanyahu afariki katika ajali


Israel imethibitisha leo kwamba muhanga wa ajali ya ndege iliyoanguka nchini Ugiriki alikuwa ni shahidi kwenye kesi inayomuhusisha waziri mkuu wake wa zamani Benjamin Netanyahu. Kauli hiyo ya Israel imetolewa wakati maafisa wa Ugiriki wakiwa wameanzisha uchunguzi kuhusu ajali hiyo. 

Afisa wa ngazi ya juu kuhusu usalama wa safari za anga wa Ugiriki Loannis Kondylis amesema kwamba mvuvi mmoja aliyeshuhudia tukio hilo karibu na kisiwa cha Samos jana Jumatatu alidai kusikia mara mbili kishindo kikubwa cha miripuko ingawa bado chanzo cha ajali hiyo hakijajulikana. 

Wizara ya mambo ya nje ya Israel imewatambua wahanga wa ajali ya ndege hiyo ya Cessna nambari C182 kuwa ni Haim na Esther Giron mtu na mkewe wenye umri wa miaka 69 kutoka mjini Tel-Aviv. 

Haim Giron, ni naibu mkurugenzi wa zamani katika wizara ya mawasiliano alipangiwa kutoa ushahidi wake katika kesi inayomuhusisha Benjamin Netanyahu. 

Netanyahu anatuhumiwa kutoa rushwa kwa matajiri wamiliki wa vyombo vya habari kwa lengo la kutaka kutangazwa kwa mazuri.

Post a Comment

0 Comments