Waziri wa zamani wa afya DRC aondolewa gerezani kwa dhamana



Waziri wa afya wa zamani wa Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo, Dkt Eteni Longondo, ameachiliwa huru baada ya kuwa kufungwa kwa siku 17 katika gereza kuu la Kinshasa.

Bw Longondo aliachiliwa kwa dhamana Jumanne, kulingana na wakili wake, Hugues Pulusi Eta.

Anakabiliwa na shutuma za ubadhilifu wa pesa kiasi cha dola milioni 6ambazo zilikuwa zimetengwa kwa jaili ya mapambano dhidi ya janga la Covid alipokuwa mamlakani kati ya tarehe 9 Septemba na tarehe 28 Aprili mwaka huu.

Aliwekwa gerezani tarehe 27 Agosti baada ya uchunguzi wa saa tano uliofanywa na ofisi ya mwendesha mashitaka.

Dkt Longondo ambaye ni mshirika wa Rais wa sasa Felix Tshisekedi, amekuwa akikana shutuma hizo dhidi yake.

Haijawa wazi ni lini kesi yake itaanza.

Mtanfulizi wake, Dkt Oly Ilunga, kwa sasa anatumikia kifungo cha miaka mitano jela, baada ya kupatikana na hatia mwezi Machi mwaka jana ya matumizi mabaya ya fedha ambazo zilipaswa kutumika katika mapambano dhidi ya mlipuko mbaya zaidi wa Ebola nchini DRC.

 

Post a Comment

0 Comments