Baraza la usalama la UN lalaani tabia ya Korea Kaskazini kufyatua makombora


Wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wamelaani tabia ya Korea Kaskazini, kufuatia majaribio ya karibuni ya makombora yaliofanywa na taifa hilo. 
 
Wawakilishi wa Ufaransa, Ireland na Estonia katika Umoja wa Mataifa, wamesema ufyatuaji wa makombora hayo ulikuwa sehemu ya mfano wa uchokozi wa Korea Kaksazini. 
 
Mabalozi hao wametoa wito kwa taifa hilo kuheshimu vikwazo ilivyowekewa na Umoja wa Mataifa. Marekani na Uingereza pia zilielezea hisia sawa. Baraza la usalama lilikutana mjini New York kujadili hali hiyo katika kikao cha faragha, lakini awali, hakukuwa na taarifa ya pamoja.

 

Post a Comment

0 Comments