Fahamu madhara ya kunywa maji ya baridi

 



Watu wengi wamekuwa na tabia ya kupenda kunywa maji yaa baridi mara kwa mara.Maji haya yamekuwa kama kiburudisho katika mazingira yenye hali ya joto (mfano Dar es salaam). Pia watu wengi hupenda kunywa maji haya pindi tu wanapomaliza kula chakula hasa muda wa mchana na jioni.

Vyakula vingi tunavyokula huwa na mchanganyiko wa mafuta. Hivyo pale unapomaliza kula chakula na kuamua kunywa maji ya baridi, maji hayo huchangia kwa kiwango kikubwa kugandisha mafuta yaliyomo kwenye chakula ulichokula.

jambo hili usababisha usagaji wa chakula tumboni kuwa wa kiwango cha chini (kwenda taratibu) ukilinganisha na wastani wake unaohitajiaka na upelekea muhusika kukosa choo mara kwa mara. Pia  ukiachana na kukosa choo madhara mengine uchukua muda mrefu kujitokeza.

Pia hali hii inapozidi kuendelea kadri muda unapozidi kuongezeka tabaka la mafuat(fats) huanza kujijenga kwenye utumbo na baada ya muda kusababisha saratani ya utumbo.

Ninaimani mpaka sasa umeanza kuona athari zitokanazo na unywaji maji baridi

Nini cha kufanya?

Anza mara moja kupunguza kutumia maji ya baridi.Ninafahamu kuacha mara moja ni jambo gumu sana kuna msemo wa kiswahili unasema "tabia ni kama ngozi".Hivyo nakushauri anza kupunguza matumizi ya maji ya baridi  kadiri siku zinavyozidi kuongezeka mpaka utakapoacha kabisa.Pia si vyema kila baada ya kula  ukanywa maji unashauriwa kusubiri baada ya nusu saa ndio unywe maji.

kuna faida za kunywa maji ya uvugu vugu?

Ndio kupendelea kunywa maji ya uvuguvugu kuna faida nyingi, moja wapo ni kusafisha tumbo lako kwa kuyeyusha mafuta pia kusaidia usagaji wa chakula tumboni na hivyo kukuwezesha kutoa sumu na uchafu mwilini kwa njia ya haja kubwa. Ukifanya hivi mara kwa mara itakuhakikishia kutokuwa na uchafu tumboni wala mrundikano wa mafuta mabaya mwilini.

Post a Comment

0 Comments