Korea Kaskazini yafanya jaribio la kombora kwa kutumia nyambizi


Korea Kaskazini imetangaza kufanya jaribio la kombora lake lililoundwa kwa namna ya kufyatuliwa kutoka katika nyambizi. ikitajwa kuwa ni silaha ya aina ya kipekee kufanyiwa majaribio katika kipindi cha miaka miwili.

Uvumbuzi wa kombora hilo unaelezwa pia unaongeza nguvu za kijeshi kwa zingatio la operesheni za chini ya maji. Televisheni ya taifa ya Korea Kaskazini imetangaza jaribio hilo linaiweka teknolojia ya ulinzi wa kijeshi katika viwango vya juu pamoja na kuwajengea uwezo wanajeshi wa majini.

Kwa upande wa taifa jirani na Korea Kaskazini, Korea Kusini limesema walibaini kufanyika kwa jaribio la kombora hilo na kwamba baada ya kufyatuliwa lilitua katika eneo la bahari lililopo kati ya Rasi ya Korea na Japan.

Jaribio hilo la Jumanne, linatajawa kuwa la tano tangu Septemba na linafanyika katika kipindi ambacho Korea Kaskazini inaongeza shinikizo dhidi ya Marekani na Korea Kusini kuachana na kile serikali hiyo inahisi sera za kihasama katika kipindi ambacho kutajawa kufanyika mazoezi ya kijeshi ya pamoja baina ya mataifa hayo. Na kadhalika vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini.

Ikulu ya Marekani, imelaani jaribio hilo. Jen Psak ni mratibu mwandamizi wa masuala ya habri wa ikulu hiyo. "Jaribio hili linakiuka maazimio mengi ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na kitisho cha kikanda. Tunatoa wito kwa serikali ya Korea Kaskazini kujitenga na vitendo vya vya kichokozi zaidi na na kushiriki katika mazungumzo endelevu na yenye uzito. Na ahadi yetu  katika kuzilinda Jamhuri ya Korea na Japan itabaki kuwa thabiti. Na fursa yetu itasalia kutoa nafasi ya kukutana popote, wakati wowote, bila ya masharti yoyote" alisema afisa habari huyo mwandamizi.

Shirika la habari la Korea Kaskazini KCNA limesema kombora hilo lilirushwa kutoka katika meli iliyopewa jina la Yagung, nyambizi ambayo Korea Kaskazini inasema imuundwa kwa ajili ya kufanyia mashambulizi ya aina hiyo na vilevile iliwahi kutumika katika jaribio lingine la kombora la 2016.

Picha ambazo zimesambazwa na taifa hilo zinaonesha kombora linaibuka kutoka majini huku likitoa moto, uliambatana na moshi mweupe mawinguni kutoka katika usawa wa bahari. Lakini pia picha nyingine ilionesha sehemu ya juu ya kile kilichoonekana kama nyambizi.

Jaribio hilo linafanyika katika kipindi cha siku chache kabla ya mwakilishi wa Marekani kwa Korea Kaskazini Sung Kim akitarajiwa kwenda mjini Seoul kwa ajili ya kujadili na washirikia wao namna ya kufufua mazungumzo ya kidiplomasia na Korea Kaskazini.

 

Post a Comment

0 Comments