Makundi ya kutetea demokrasia Eswatini yakataa miito ya mazungumzo

 


Serikali ya Eswatini imetoa wito wa utulivu na mazungumzo kufuatia ziara ya wapatanishi wa kikanda wanaojaribu kuutatua mzozo wa mkubwa wa kisiasa uliosababisha vurugu mbaya, lakini vyama vya upinzani na asasi za kiraia, zimekataa miito ya mazungumzo. 

Wapatanishi kutoka jumuiya ya maendeleo ya nchi 16 za kusini mwa Afrika, SADC, siku ya Ijumaa walihitimisha siku mbili za mazungumzo na mfalme wa taifa hilo Mswati wa Tatu. 

Katika taarifa hapo jana, mkuu wa ulinzi na masuala ya kisiasa wa Jumuiya hiyo, Ris Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini, aliunga mkono wazo la mazungumzo ya kitaifa. 

Ramaphosa alitoa wito wa utulivu na heshima kwa utawala wa sheria na haki za binaadamu kutoka pande zote mbili ili kuwezesha kuanza kwa mchakato huo. 

Polisi inasema kuwa watu 37 wameuawa tangu kuzuka kwa maandamano dhidi ya uongozi wa taifa hilo mnamo mwezi Juni yaliyochochewa na wananchi kutoridhishwa na hali ya maisha na ukosefu wa uhuru wa kisiasa.


Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi