Uingereza inasema muda unayoyoma kwa suluhisho kuhusu mazungumzo ya Brexit

 


Serikali ya Uingereza inajaribu kuharakisha kasi ya mazungumzo kutatua utata wa kibiashara kati yake na Umoja wa Ulaya baada ya taifa hilo kujiondoa katika Umoja huo, lakini imesema bado pande hizo mbili zinatafautiana vikali na muda wa kutatua tafauti hizo unayoyoma.

Wajumbe wa Uingereza na Umoja wa Ulaya wamekutana mjini Brussels katika muda wa wiki iliyopita kujaribu kutatua tofauti kubwa zilizojitokeza kuhusiana na sheria za biashara kwa Ireland ya Kaskazini. 

Mazungumzo hayo yataendelea mjini London siku ya Jumanne huku Uingereza ikisema kuwa bado kuna mapengo makubwa katika masuala muhimu.

Serikali ya Uingereza imesema kuwa kufikia sasa mazungumzo yamekuwa ya tija, lakini ikaongeza kuwa inahitaji kuona ufanisi hivi karibuni badala ya kukwama katika mchakato wa mazungumzo yasiyokuwa na mwisho kwa sababu masuala yaliyoko kuhusu Ireland ya Kaskazini bado hayajatatuliwa.


Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi