Marekani yaihimiza Korea Kaskazini kurudi kwenye mazungumzo

 


Mwanadiplomasia mkuu wa Marekani ameihimiza Korea Kaskazini kujiepusha na majaribio ya mapya ya makombora na kurudi tena katika mazungumzo ya kidiplomasia ya nyuklia. 

Afisa mkuu wa Marekani kuhusu masuala ya Korea Kaskazini Sung Kim baada ya kukutana na maafisa wa Korea kusini kujadili masuala ya matukio ya hivi karibuni, ametoa wito kwa Korea Kaskazini kuacha uchokozi na shughuli zitakazoleta ukosefu wa amani. 

Kim amesema Marekani ipo tayari kushiriki mazungumzo bila masharti na kwamba haina dhamira ya uadui kwa Korea Kaskazini. 

Jumanne iliyopita, Korea Kaskazini ilirusha kombora jipya la masafa marefu kutoka kwenye manowari katika duru yake ya tano ya majaribio ya silaha katika wiki za hivi karibuni.


Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi