Rais Museveni: Shambulizi la Kampala ni "kitendo cha Ugaidi"

 


Polisi nchini Uganda imesema mtu mmoja ameuwawa na wengine 7 kujeruhiwa katika mlipuko mkubwa katika mji mkuu Kampala. 

Tukio hilo ambalo Rais Yoweri Museveni amelitaja kuwa la kigaidi, linaripotiwa kutokea majira ya saa tatu usiku wa kuamkia leo katika mgahawa maarufu ulioko mtaa wa Kawempe kaskazini mwa Kampala. 

Msemaji wa Polisi Fred Enanga kupitia taarifa aliyoiandika kwenye mtandao wa Twitter, amethibitisha tukio hilo na kusema majeruhi wamepelekwa katika hospitali ya rufaa ya Mulago wakiwa na majeraha mabaya. 

Polisi hata hivyo imewataka raia kuwa watulivu hadi chanzo cha mlipuko huo kitakapobainika. Rais Yoweri Museveni ametaja tukio hilo kuwa la kigaidi na kuahidi kuwasaka wahusika.


Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi