Oct 13, 2021

Mkuu wa WHO ahimiza ugawanaji wa chanjo ya covid-19 kufanikisha lengo

  Muungwana Blog 2       Oct 13, 2021

 


Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Afya Duniani WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus, hii leo ameyahimiza mataifa na makampuni yanayodhibiti ugavi wa chanjo cha ugonjwa Covid-19 kutoa kipaumbele kwa mpango wa kimataifa wa ugawanaji chanjo COVAX, ili kufikia malengo ya utoaji wa chanjo. 

Tedros amesema katika mkutano na waandishi habari kwamba wanashirikiana na viongozi kuunga mkono utoaji kipaumbele na upangaji unaohitajika kufanikisha lengo la kuchanja asilimia 40 ya wakaazi wa dunia, kwa kuchukuwa hatua kubwa na madhubuti.


logoblog

Thanks for reading Mkuu wa WHO ahimiza ugawanaji wa chanjo ya covid-19 kufanikisha lengo

Previous
« Prev Post

No comments:

Post a Comment