Oct 14, 2021

Mshambuliaji wa upinde na mshale aua watano Norway

  Muungwana Blog 3       Oct 14, 2021

Mshambuliaji aliyejihami kwa upinde na mishale amewaua watu watano katika jengo la maduka nchini Norway. Mtu huyo anashikiliwa na polisi kwa mahojiano zaidi kuhusu shambulizi hilo.

Mshambuliaji huyo aliwafyatulia mishale watu waliokuwa katika jengo la maduka lililopo katika mji mdogo ulio karibu na mji mkuu wa Norway, Oslo.

Mkuu wa polisi katika jamii ya Kongsberg, karibu na Oslo amesema bila ya kutoa maelezo zaidi kwamba kulikuwa na makabiliano kati ya maafisa wa polisi na mshambuliaji huyo.

Watu wengine wawili walijeruhiwa na kulazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi, ikiwa ni pamoja na afisa ambaye hakuwepo kazini na mwingine aliyekuwemo ndani ya duka.

Kaimu waziri mkuu wa Norway Erna Solberg amelielezea shambulizi hilo kuwa ni kutisha na kusema ilikuwa ni mapemamno kubashiri nia ya mshambuliaji huyo.

Mshambuliaji huyo anashikiliwa na polisi na hakuna msako wa mtu mwingine anayedhaniwa kuhusika kwenye shambulizi hilo.

 

logoblog

Thanks for reading Mshambuliaji wa upinde na mshale aua watano Norway

Previous
« Prev Post

No comments:

Post a Comment