Australia yaliorodhesha kundi lote la Hezbollah kuwa taasisi ya kigaidi


Australia leo imeorodhesha kundi la Hezbollah kuwa la kigaidi na kupanua marufuku iliyowekwa dhidi ya vikundi vyenye silaha vyenye mafungamano na kundi hilo lenye ushawishi mkubwa nchini Lebanon.


Waziri wa Mambo ya Ndani nchini humo Karen Andrews amesema kundi hilo la Washia wanaoungwa mkono na Iran linaendelea kutishia kufanya mashambulizi ya kigaidi na kutoa msaada kwa mashirika ya kigaidi hali inayoleta kitisho halisi na cha kuaminika kwa Australia.


Matthew Levitt, afisa wa zamani wa Marekani katika kitengo cha kukabiliana na ufadhili wa ugaidi, ameliambia shirika la habari la Ufaransa AFP kwamba hatua hiyo ilipaswa kuchukuliwa muda mrefu uliopita. 


Mnamo mwezu Juni, alitoa ushahidi kwa bunge la Australia na kusema kwamba jinsi kundi hilo lilivyokuwa limeorodheshwa awali haikutosha na kuongeza kuwa kundi la Hezbollah lina muundo na kufanya kazi kama shirika moja

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items