Ticker

6/recent/ticker-posts

Burhani awafuta kazi maafisa waandamizi wa usalama wa taifa

 


Kiongozi mkuu wa jeshi wa Sudan, Jenarali Abdel Fattah al-Burhan, amewafuta kazi majerali wanane, ambao ni maafisa wa intelijensia na kumbadilisha mkuu wa usalama wa taifa. 


Habari hiyo ni kwa mujibu wa shirika la habari Reuters ambalo limevinukuu vyanzo viwili tofauti.


Taarifa hii inafuatia kuteuliwa kwa mkuu mpya wa usalama wa taifa, ikiwa ni wiki moja baada ya jeshi kufikia makubaliano ya kumrejesha katika wadhifa wake Waziri Mkuu Abdallah Hamdok, ambaye aliwekwa katika kizuizi cha nyumbani, baada ya mapinduzi ya Oktoba 25.

Post a Comment

0 Comments