Meneja wa timu ya taifa ya Uingereza Gareth Southgate ametia saini kandarasi mpya itakayomweka kwenye nafasi hiyo hadi Disemba 2024.
Southgate, ambaye mkataba wake wa awali ulitarajiwa kumalizika baada ya Kombe la Dunia la majira ya baridi ya 2022 nchini Qatar, amekuwa meneja wa timu ya taifa tangu Novemba 2016.
Aliiongoza Uingereza kufika fainali ya Euro 2020 – hatua bora zaidi kwa timu ya wanaume katika miaka 55 - mwezi Julai.
"Inasalia kuwa fursa ya ajabu kuiongoza timu hii. Tuna nafasi kubwa mbele yetu," alisema.
Southgate atasimamia matayarisho ya England katika Kombe la Dunia mwaka ujao, ambalo litaanza Novemba 21-18 Desemba, na hatua za kufuzu kwa Euro 2024, na michuano hiyo itafanyika kutoka 14 Juni-14 Julai.
Meneja msaidizi Steve Holland pia amekubali mkataba mpya hadi mwisho wa 2024.