Israeli Kuruhusu Wayahudi 3,000 wa Ethiopia Kuhamia nchini humo


Serikali ya Israel siku ya Jumapili iliidhinisha uhamiaji wa maelfu ya Wayahudi kutoka Ethiopia inayokumbwa na vita, ambao baadhi yao wamesubiri kwa miongo kadhaa kuungana na jamaa zao nchini Israel.


Uamuzi huo ulichukua hatua kuelekea kusuluhisha suala ambalo kwa muda mrefu limetatiza uhusiano wa serikali na jamii ya Ethiopia nchini humo


Wayahudi wa Ethiopia wapatao 140,000 wanaishi Israeli. Viongozi wa jamii wanakadiria kuwa takriban wengine 6,000 wamesalia nyuma nchini Ethiopia.


Ingawa familia hizo ni za asili ya Kiyahudi na wengi wao ni Wayahudi, Israeli haiwaoni kuwa Wayahudi chini ya sheria za kidini. Badala yake, wamekuwa wakipigania kuingia nchini chini ya mpango wa kuunganisha familia ambao unahitaji idhini maalum ya serikali.


Wanaharakati wa jamii wameishutumu serikali kwa kujikokota katika kutekeleza uamuzi wa 2015 wa kuwaleta Waethiopia wote waliosalia wa ukoo wa Kiyahudi nchini Israeli ndani ya miaka mitano.

Post a Comment

0 Comments