Kesi inayomkabili mfanyabiashara Tarime yaanza kusikilizwa na Mahakama kuu kanda ya Musoma.

 


Na Timothy Itembe Tarime.

Mfanyabiashara anayefahamika kwa Jina la Lucas Sotel kesi yake imenza kusikilizwa na Mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Musoma Mkoani Mara chini ya Mh ,Jaji mfawidhi John Kahyoza.

Akiwasilisha shauri hilo wakili wa serikali Yese Temba mbele ya mahakama kuu kanda ya Musoma iliyokalia wilayani Tarime alisema kuwa kesi hiyo ina mashahidi wapatao watano.


Temba aliwataja mashahidi kuwa ni pamoja na Magoiga Joseph,Ryoba Mulange,Matutu Range ambaye kwasasa Alisha fariki Dunia,Benard Otieno Makonyo Daktari na askari Polisi F,4397koplo Mstapha wa kituo cha polisi Sirari.


Mfanyabiashara,Lucas Sotel anakabiliwa na kesi ya mauaji ambayo ni kinyume cha sheria kifungu cha 1996 na 1997, kanuni ya adhabu sura namba 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2019.


Awali wakili huyo aliiambia mahakama kuwa mashahidi tayari wamepewa wito wa mahakama ili kuhudhuria mahakama hiyo kwa ajili ya kutoa ushahidi juu ya mwenendo wa kesi hiyo lakini mpaka kesi inaanza kusikilizwa mashaidi hawakuwepo mahakamani hapo ndipo Mh: Jaji alihairisha kusikiliza kesi hiyo kwa muda.


Mauji ya kijana Wankuru Nyamuhanga mkazi wa kijiji cha Buriba wilayani Tarime Mkoani Mara yanadaiwa kutendeka mnamo Agosti 9 Mwaka 2014 katika kijiji cha Buriba.


Baada kuhairisha kesi hiyo ilianza kusikilizwa tena kwa mara ya pili ambapo Mashahidi wawili kwa upande wa Jamhuri kati ya watatu ambao walipaswa kuwa mahakamani hapo walitoa ushahidi wao.


Kati ya Mashahidi hao shahidi mmoja ambaye alipewa wito na mahamama hiyo nakusaini wito nakushindwa kufika mahakamani hapo wakili wa Serikali aliomba mahakama kutoa hati ya kukamatwa kwa shahidi huyo ambapo Mh Jaji mfawidhi Mahakama kuu kanda ya Musoma,John Kahyoza aliagiza kukamatwa mara moja kwa shahidi huyo ili aweze kuja na kutoa ushahidi mahakamani hapo.


Vilevile Jaji alisisitiza washauri wa mahakama kusaidia mahakama katika utoaji wa hukumu juu ya kesi hiyo na siyo kusikiliza ushahidi unatajwa mtaani bali wasikilize ushaidi unaotolewa mahakamani hapo.


Mshitakiwa Lucas Sotel anatetewa na mawakili wawili ambao ni Tumaini Kigombe (Sayari) na Selina Magoiga, Wakili Kigombo wakati akiuliza maswali kwa mashahidi hao wote wawili mbele ya mahakama,mashahidi wote kwa nyakati tofauti walikiri kutomtambua ambaye anadaiwa kumuua kijana Wankuru Nyamohanga ambaye kwa sasa ni Marehemu.


Baada ya kusikiliza ushahidi huo Mahakama haikuwa na maswali kwa mashahidi hao ambapo Jaji Kahyoza alihairisha kesi hiyo nakuwa itakuja kisikilizwa tena Novemba 29 mwaka huu.

Post a Comment

0 Comments