Marekani itaanza tena mazungumzo na kundi la Taliban wiki ijayo nchini Qatar, kushughulikia miongoni mwa masuala mengine mapambano dhidi ya ugaidi na mzozo wa kibinadamu nchini Afghanistan.
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje Ned Price amesema kuwa ujumbe wa Marekani utaongozwa na mjumbe maalumu wa Marekani kwa Afghanistan Tom West katika mazungumzo hayo ya wiki mbili.
Price ameongeza kuwa pande hizo mbili zitazungumzia masuala muhimu ya maslahi kwa mataifa hayo ambayo ni pamoja na oparesheni za kukabiliana na ugaidi dhidi ya kundi linalojiita Islamic State, IS na Al-Qaeda, usaidizi wa kibinadamu, uchumi ulioharibiwa wa Afghanistan, na kuondoka kwa usalama kwa raia wa Marekani na na Waafghanistan walioifanyia kazi Marekani wakati wa vita vya miaka 20 nchini Afghanistan.
Wiki mbili zilizopita, West alikutana na wawakilishi wa kundi la Taliban nchini Pakistan.