Mazungumza ya nyuklia ya Iran kuanza Vienna, Austria


Mazungumzo ya mzozo wa nishati ya nyuklia, yenye lengo la kuyaokoa makubaliano ya 2015 kati ya Iran na mataifa yenye nguvu yanatarajiwa kuanza leo mjini Vienna Austria.


Mazungumzo hayo yanaanza wakati ambapo Iran inaendelea kushikilia msimamo wake mkali, huku mataifa ya Magharibi yakionekana kuendelea kuvurugikiwa na matumaini ya mafanikio yakisalia kuwa madogo.


Wanadiplomasia wanasema muda umepotea sana katika jitihada za ufufuzi wa mkataba huo, ambao mwaka 2018 rais aliyepita wa Marekani Donald Trump aliikasirisha Iran kwa kuutelekeza mkataba huo na kuyafedhehesha mataifa mengine yanayohusika ambayo Uingereza, China, Ufaransa, Ujerumani na Urusi.


Duru ya sita ya mazungumzo kama hayo ilifanyika Aprili na June. Na hii ya sasa inaanza baada ya kusitishwa kulikotokana na uchaguzi wa rais uliomwingiza madarakani rais mpya wa Iran Ibrahim Raisi.

Post a Comment

0 Comments